Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Kimataifa ya SShirika la Habari la Hawza, hivi karibuni baadhi ya watafiti wa elimu za dini na mashaykh wa madhehebu ya Tijaniyya kutoka Senegal, katika muktadha wa safari ya da‘wa kwenda nchini Algeria, walikutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Muhammad al-‘Id at-Tijani, Murshid wa Tariqa ya Tijaniyya katika eneo la Al-Tamasin la nchini humo.
Katika mkutano huo, Sheikh Muhammad al-‘Id at-Tijani, akieleza furaha yake kwa uwepo wa watafiti wa Senegal, alielezea mkutano huo kuwa ni wa kujenga sana, na akaongeza: Algeria na Senegal, kama nchi mbili rafiki tangu zama za kale hadi leo, zimekuwa zikihifadhi idadi kubwa ya wapenzi na wanafunzi wa Tariqa ya Tijaniyya, na mikutano ya aina hii —kwa kuwa huchangia kuimarisha tariqa — ni ya lazima na inapaswa kupewa kipaumbele.
Ni lazima kuelezwa kuwa, eneo la Tamasin, au Dairat al-Tamasin, ni miongoni mwa maeneo yenye hali ya hewa kame na joto kali nchini Algeria. Eneo hili liko katika mkoa wa Wargla (Ouargla) mashariki mwa nchi hiyo, na linapatikana katika ukanda wa mpaka wa Jangwa la Magharibi unaokaribiana na nchi ya Morocco. Jumla ya wakazi wake, wanaokadiriwa kuwa takribani watu elfu hamsini, wote ni Waislamu wa madhehebu ya Tijaniyya. Aidha, majengo mengi na alama za kihistoria zilizobaki tangia kipindi cha utawala wa Wafatimiyun (Fatimiyya) wa madhehebu ya Kishia huko Afrika ya Kaskazini bado zinapatikana katika eneo hili.





Maoni yako